- Vitu muhimu vya kuzingatia unapotaka kununua simu ya Mkononi - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

SIMU

Vitu muhimu vya kuzingatia unapotaka kununua simu ya Mkononi

on

Je, unatumia njia gani za kujua na kuchagua simu unayotaka kwa haraka? Simu hizo sasa zipo za kila aina na kila bei. Samsung, Lumia, Huawei, Tecno ni majina machache kati ya mengine yanayotamba Tanzania.

1. Uhifadhi (Storage) 

Simu nyingi zina uwezo wa kupokea memori-kadi ili kuongeza hifadhi ila ukubwa wa hifadhi ya ndani ya simu ni muhimu zaidi, kwani unakuonesha uhuru wako wa kushusha programu na mara ngapi utahitaji kufuta au kuhamisha vitu kutoka kwenye simu yako. Kama wewe ni mtu wa kutumia apps nyingi na unapenda uhuru huo, epuka simu zenye hifadhi ya ndani chini kama 4GB. Tumezungumzia kipindi cha nyuma jinsi Samsung, Google na Apple wanavyozidi kujisombea wateja kwa kuwapa hifadhi-pepe. Hii inaonyesha mtindo mwingine wa hifadhi. Unaweza pia kuangalia kiasi gani cha hifadhi-pepe unapewa na simu yako kama ziada.

2. Kumbukumbu/RAM 

 Kumbukumbu ni moja ya mambo yanayobana kasi ya simu yako kwenye kuendesha programu. Katika soko la sasa, kumbukumbu ya 512 – 800MB utaipata hadi Tsh 200, 000. Kumbukmbu ya uhakika ya 1GB inapatikana kwenye simu za bei ya kati inayoambaa-ambaa hadi Tsh 600, 000. Kumbukumbu ya 2GB+ ni bora zaidi na inapatikana kwenye simu za hali ya juu kama Samsung Note na Nexus 6. Apple i-phone 6 ina kumbukumbu ya 1GB na simu za Windows huwa na RAM ndogo pia kwa kuwa hutumia kumbukumbu kidogo zaidi ya mfumo wa Androidi. 

3. Prosesa 

Prosesa ni sehemu muhimu inayobana mambo mengi ikiwemo jinsi simu inavyomudu rangi, chaji ya betri na kasi ya kuendesha programu. Prosesa zinapambanishwa kwa kipimo cha GHz, ambapo namba kubwa zaidi inaonesha uwezo mkubwa na kasi zaidi. Prosesa vinazotamba kwa kasi sasa hivi ni za Snapdragon, Exynos, A8 ya Apple na MediaTek. Na katika hizo, kuna aina nyingi: Quadcore Snapdragon 801, 805, Apple A7. Inafaa ulize ipi inayotamba sokoni kila wakati kwa sababu zinatengenezwa kwa kasi sana. 

4. Betri na Chaji 

Teknolojia ya betri inatabiriwa na baadhi ya watu wa teknolojia kukuwa kidogo sana licha ya jitihada za karibuni zilizotoa betri zilizopungua ukubwa na zinazochaji haraka, na hata kuongeza usalama wa hizi betri. Unaponunua simu angalia uwezo wa kukaa na chaji(unaopimwa kwa mAh) na teknolojia ya betri. Betri za mhA 2000 na kuendelea zitakupa muda kuanzia masaa sita ya chaji ukiwa unaitumia simu sana. Chini ya hapo unahitaji uvumilivu wa kutosha wa kutembea na chaja au betri ya ziada.

 5. Mfumo-endeshaji 

Kwa sasa, soko limetawaliwa na Android, IOS na Windows huku BlackberryOS na mifumo mingine ikijitahidi kubaki. Siku za karibuni, moja ya wakubwa wa Blackberry amekaririwa akilalamika kuhusu mfumo wake kukosa mvuto wa watengenezaji wa apps muhimu na hivyo kuleta wasiwasi kwa watumiaji wa Blackberry kubaki na mfumo huo. Ni jambo muhimu sasa kuangalia mfumo gani unakufaa na sifa zake. Windows inasifiwa kwa kutengenezwa vizuri (‘hardware build’), Android inasifiwa kwa uhuru wa kuifanya utakavyo na kubadilisha muonekano wake utakavyo. Simu za Apple zinasifiwa kwa kuwa na kiwango na mvuto wa kipekee. Blackberry yenyewe inapendwa na wafuasi wake kwa sababu ya kibodi yake na upekee wa aina yake. Unaweza pia kujaribu mifumo inayokuja ya FirefoxOS na Ubuntu-phone ambayo labda inaweza kubadili soko katika miaka ya karibuni. 

 6. Ukubwa na Uhalisia wa Skrini 

 TFT, IPS, Retina Display na True HD ni majina machache ya mauzo kati ya majina ya skrini nyingi duniani. Je, unajua skrini bomba kwa sasa? – Jibu ni skrini yoyote yenye ukubwa wa kuanzia inchi 4.5! Hili ni kutokana na wachambuzi wengi na hata ukiiangalia simu zinazoingia sokoni sasa hivi. Watu wanataka kuona kioo kikubwa, siyo kuchungulia skrini tena. Kama unapenda rangi na uhalisia na pia kudumu, skrini bomba kabisa zinapatikana kuanzia laki 3.5 kwa simu ya S3, kwa sasa, ila chini ya hapo, hamna tofauti sana.. 

7. Uwezo wa Kamera 

Kamera ni kitu cha msingi sana kwenye uchaguzi wa simu siku hizi. Umuhimu wake umekuzwa na matumizi ya mitandao ya jamii amabayo imeleta urahisi wa kusambaza picha hizo kwa watu wetu wa karibu. Hilo linaonekana kuleta furaha na kuongeza upendo kirahisi. Mbali na hilo, kamera zinatumika kutunza kumukumbu na nyaraka katika kazi na masomo. Kipimo kirahisi cha ubora wa kamera kinachotumika ni ukubwa wa Mega-pixeli (wingi wa vipisi vya picha ndani ya picha) ila kuna vipimo vingine muhimu zaidi kama ubora wa lens, ubora wa sensa, ambayo ndio inayopokea picha na suala la ‘image stabilization technology’ ambayo inapunguza ubovu wa picha kutokana na kutingisha mkono. Ni vyema ukachunguza ubora wa vipimo hivyo kwenye simu husika. Kwa sasa, simu yenye kamera nzuri inategemea sana na pesa yako ila kwa muongozo wa kawaida, simu za Lumia zinakuwa na kamera nzuri kwa bei kidogo zaidi ya mifumo mingine.

8. Upya na Ubora wa simu 

Watu wengine huchagua simu kutokana na sifa ya upya. Sabababu kuu ikiwa ni kupata kifaa kilicho imara na ubora zaidi..

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!