- Ufahamu mfumo wa malipo kielekroniki kupitia Wakala wa Tehama wa Serikali (E-government) - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

UCHAMBUZI

Ufahamu mfumo wa malipo kielekroniki kupitia Wakala wa Tehama wa Serikali (E-government)

on

Taarifa kutoka ndani ya taasisi ya Wakala ya Serikali Mtandao Mtandao (e-Government Agency), zimeeleza kuwa wao kutengenezwa kwa mfumo huo ulikuwa mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita.

Chanzo hicho cha habari kinaeleza kuwa baada ya kuelekeza mpango huo kwa serikali Wizara ya Fedha ndiyo watakaokuwa wasimamizi wakuu.

Baadhi ya mashirika yameshaanza kutangaza huduma hizo kwa wateja wake ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo nalo limejiunga Aprili 1, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Leila Muhaji, wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) wameunganishwa  .

“Kuanzia Aprili 2, mwaka huu Tanesco imehamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG) kama matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali.

“TANESCO ikiwa miongoni mwa taasisi za Serikali, itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi za TANESCO, kampuni za simu pamoja na Benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki,’’ alieleza Leila katika taarifa hiyo.

“Pia Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa shirika hilo la umeme watahakikisha mfumo huo unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU,” alisema.

Hadi sasa taasisi nyingine za Serikali ambazo zimeanza kutumia mfumo huo kwa mafanikio ni Polisi, Brella, Wizara ya Ardhi, TRA pamoja Dawasco.

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!