- Simu ya kwanza inayoweza kuoshwa kwa Maji na sabuni - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

SIMU

Simu ya kwanza inayoweza kuoshwa kwa Maji na sabuni

on

Mambo vipi Rafiki? Naamini wengi wetu tunaamini simu zetu zikiingia maji basi litakuwa tatizo lakini kwa jinsi Teknolojia inavyozidi kukua kila kukicha, ndivyo tunavyozidi kupata vitu vya aina mbalimbali na vya kustajabisha, kama simu hii ya kwanza kutengenezwa ambayo inaweza kuoshwa na sabuni, simu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya kijapani ya KDDI simu hiyo inayo kwenda kwa jina la “Digno rafre” inategemewa kuzinduliwa siku chache zijazo. Ndio zipo simu janja nyingi ambazo zinauwezo wa kuzuia maji kuingia ndani ya simu lakini hii itakuwa ni simu ya kwanza ambayo itaweza kusio tu kuzuia maji kuingia ndani bali hata kama utataka kuiosha na sabuni basi utaweza kufanya hivyo bila kuwa na wasi wasi na kuiharibu.

Simu hiyo inayotegemewa kuuzwa kwa karibu dola 175 za kimarekani (Takribani laki nne za sh) na pengine itauzwa Japani tu kwa sasa. Watengenezaji wa simu hii wanawalenga hasa wazazi ambao wanawatoto wadogo ambao ni rahisi kuchafua simu zao. Simu hiii hata hivyo itaweza kuhimili kuoshwa na baadhi ya sabuni sio kila sabuni, katika tangazo ambalo watengenezaji wa simu hiyo wameliweka mtandaoni mtoto

anadondosha simu katika chakula na mama yake anaonekana akiiosha katika bomba na sabuni kisha baadaye mtoto anaonekana akichezea simu bafuni. Teknoloji inayotumika hapa ni ile ya kuzuia maji kuingia ndani ya simu lakini imeongezwa pia uwezo wa kuzuia povu na sabuni, screen yake kwa upande mwingine ni kwamba inaweza kutumiwa hata na mikono mibich

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!