- Sababu 3 za watumishi wa umma kutotumia mitandao ya kijamii wakati wa kazi nchini Tanzania - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

MITANDAO

Sababu 3 za watumishi wa umma kutotumia mitandao ya kijamii wakati wa kazi nchini Tanzania

on

Serikali ya Tanzania kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali wakati wa kazi, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasi

Mitandao ya kijamii haitapatikana kwenye intaneti ya serikali wakati wa muda wa kazi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri,” kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu (Utumishi), Dkt. Laurean Ndumbaro.

Aidha, Dkt Ndumbaro amesema kwamba taasisi zenye mahitaji maalum ya matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa muda wa kazi ziwasilishe maombi kwa Katibu Mkuu (Utumishi) wakiainisha watumishi wanaohitaji huduma hiyo na sababu za mahitaji hayo.

Hizi ndio sababu zilizopelekea kufungia matumizi ya mitandao ya kijamii kwenye intaneti ya serikali 

1. Watumishi wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kutekeleza majukumu yao

2. Kasi ya mtandao wa Serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususan inayopakua video, mfano “YouTube” na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia mtandao wa intaneti wa Serikali katika kutekeleza majukumu yao kuathirika

3. Upakuaji wa nyaraka zenye hatimiliki bila idhini ya wamiliki kwa kutumia Intaneti ya Serikali kinyume na utaratibu

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Yassir Oyo

Yassir Oyo

Ni Mwandishii wa Taarifa za Teknolojia kwa lugha ya kiswahili katika Mtandao wa Taarifa za Teknolojia - TeknoTaarifa. Naishi Nairobi Kenya, Napenda Teknolojia, Naipenda lugha ya kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!