- Mambo 5 yanayoweza kuwakera wengine unapokuwa unatumia simu - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

UCHAMBUZI

Mambo 5 yanayoweza kuwakera wengine unapokuwa unatumia simu

on

Simu zetu haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika 12, kwa mujibu wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Uingereza, Ofcom.

Ni mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo tunakudokeza sheria tano za matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini.

1.Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula

Watu wengi hufanya hivyo, na zaidi ya 26% ya vijana wanakubali suala hili, Kwani Simu zinapaswa kuwa zimezimwa saa zote wakati wa chakula, mikutano na sherehe. Hata kutazama televisheni inakuwa imezimwa kwa baadhi ya watu wakati mkiwa kwenye meza ya chakula.

Zaidi ya watu wanne kati ya watano walio na umri wa miaka 55 na zaidi wanafikiri haikubaliki kutazama ujumbe wa simu au kuongea na simu wakati wa kula ukilinganisha na 46% ya umri wa miaka 18 mpaka 34.

2. Kuzungumza na simu wakati unamsikiliza mtu mwingine

Kutuma ujumbe na kuzungumza wakati unazungumza na mtu uliyekaribu nae ni tabia mbaya sana, Kwani inaondoa hali ya kufahamu kitu unachosikiliza kutoka kwa mtu aliyekaribu nawe.

3. Kusikiliza muziki wenye sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma

Kitaalamu huitwa sodcasting yaani tabia ya kusikiliza muziki kutoka kwenye simu au vifaa vingine kwa sauti kubwa bila kujali wanaokuzunguka.Inahusisha kutazama video au kucheza michezo ya kwenye simu kwa sauti kubwa. 76% kati yetu tunalipinga lakini hatuachi tabia hiyo.

4. Kutembea huku ukitazama simu yako

Huinamisha vichwa, macho yakiwa kwenye kioo cha simu, wanakuja upande ambao upo.Kimoyomoyo unapiga kelele tazama mbele! tazama mbele!

5. Kutazama simu yako wakati ukiwa na wengine.

Kati ya watu 10, wanne (41%) ya watu wazima wanaona kuwa haikubaliki kutumia simu wakati uko na familia, Rafiki ndugu na jamaa mkiwa mmekaa sehemu kama kwenye sofa mkitazama televisheni au mkijadili jambo fulani.

 

 

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Yassir Oyo

Yassir Oyo

Ni Mwandishii wa Taarifa za Teknolojia kwa lugha ya kiswahili katika Mtandao wa Taarifa za Teknolojia - TeknoTaarifa. Naishi Nairobi Kenya, Napenda Teknolojia, Naipenda lugha ya kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!