- Malengo (6) yaliyowekwa na WhatsApp kwa wanaojiunga kwenye Makundi - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

MITANDAO

Malengo (6) yaliyowekwa na WhatsApp kwa wanaojiunga kwenye Makundi

on

Kila grup la WhatsApp uwa linataratibu na kanuni zilizo wekwa Lakini hali inakuwa tofauti kwa sababu wengi wanashindwa kufuata kanuni walizojiwekea. Hii inatokea pale ambapo mtu anaingiza maongezi ambayo sio muhimu kwa wakati huo au kuleta ujumbe ambao mahali alipotuma si sahihi.

1. Mkuu wa Kundi

Mkuu wa kundi ndio ana mamlaka yote .Hivyo yeye ni muhimu kuweka kanuni zote zitakazoliongoza kundi.

Haitakiwi kuwepo kwa majadiliano baina ya mtu na mtu kwa sababu makundi haya yanajumuisha mawasiliano ya kikundi na sio ya mtu mmoja moja hivyo watu wawili wakiongea masuala yao peke yao kwenye kundi maongezi hayo yanaweza kuwakera wengine.

2. Kwenye kundi la Whatsapp wana kikundi wanatakiwa kuweka ujumbe ambao unaweza kuwavutia kila mjumbe wa kundi hilo au unaweza kumfurahisha.

Suala la pili ni kwamba suluhisho ni rahisi ili kuepukana na usumbufu ambao unaweza kuwasababishia watu wengine kwa kumuandikia ujumbe binafsi mtu uliyemlenga na sio kwenye kundi.

3. Hakikisha kwamba unatuma ujumbe sahihi katika kundi sahihi

Unaweza kuhakikisha mara ya kwanza na ya pili na hata mara ya tatu kabla hujabonyeza kitufe cha kutuma ujumbe.

Kwa sababu usipokuwa makini unaweza kujiaibisha na hata kukupelekea kujitoa kwenye kundi na kuwakwepa watu kwa muda ukifikiria aibu uliyoituma katika kundi la whatsapp.

 4. Usiandike maelezo marefu

Andika maneno kwa ufupi isizidi hata sentensi moja au maneno kumi.

5. Usiwe mjumbe ambaye huchangii mijadala inayoibuka katika kundi.

Katika makundi ya whattsap hakuna nafasi ya watu ambao hawashiriki katika kuchangia maelezo yoyote pale wanapopokea ujumbe na kuusoma bila kujibu

Hii inaleta ugumu pale ambapo wajumbe wengine kwenye kundi wanasubiri majibu kutoka kwa kila mmoja lakini wengine wanakaa kimya.

6. Muombe idhini mtu kabla ya kumkaribisha katika kundi

Hivi inawezekana kweli kuwakaribisha watu thelathini katika nyumba yako bila kuwafahamu,kiuhalisia jambo hilo haliwezekani,vivyo hivyo na kwenye makundi ya whatsapp ni lazima watu kuulizwa kama atapenda kujumuika kuwa miongoni mwa wana kikundi.

Na vile vile pale unapoondoka katika kundi ni vyema kusema sababu iliyopelekea ufanye uamuzi huo.

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!