- Kama unatumia Pattern kwenye simu yako ya Android Fahamu siri hii - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

SIMU

Kama unatumia Pattern kwenye simu yako ya Android Fahamu siri hii

on

Mfumo wa Android ni njia maarufu ya kuweza kutoa ulinzi (lock) katika simu ni kwa kutumia ‘Pattern’ ambapo njia hii inasemekana sio ya kiusalama sana kama vile watu wanavyofikiria. Yaani kati ya kutumia Pin na Pattern ni bora mtumiaji wa Android atumia Pin ili kujihakikishia usalama wa hali ya juu.

Wataalamu wa ulinzi na usalama wa Marekani, Naval Academy wamefanya utafiti ambao umebainisha hilo pamoja na kushirikiana na chuo kikuu cha  Maryland Baltimore County. Katika utafiti huo iligundulika kuwa ni rahisi sana kushika Pattern za simu ya mtu pindi akiwa anafungua simu yake kuliko yule ambae anatumia Pin.

Kumbuaka katika Pattern ni rahisi sana kuweza kufuatilia njia ambayo mtu anapita katika kukamilisha Pattern hiyo lakini Pin ni ngumu kidogo kwani anarukaruka tuu.

Kama ni mtumiaji wa Android, fanya juu chini uachana na kutumia ‘Pattern’ na uhamie katika ‘Pin’ tena utumie zile zenye tarakimu sita kwa usalama zaidi. Lakini vilevile labda dunia inapokwenda sasa hivi kutakua hakuna haja tena ya kuwa na ‘Pattern’, kwa sasa simu zinatolewa loki kwa kutumia alama za vidole vile vile hata kwa uso (iPhone X).

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Yassir Oyo

Yassir Oyo

Ni Mwandishii wa Taarifa za Teknolojia kwa lugha ya kiswahili katika Mtandao wa Taarifa za Teknolojia - TeknoTaarifa. Naishi Nairobi Kenya, Napenda Teknolojia, Naipenda lugha ya kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!