- Kama siyo mtu mweusi tusingekuwa na teknolojia ya simu za mkononi - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

SIMU

Kama siyo mtu mweusi tusingekuwa na teknolojia ya simu za mkononi

on

Sekta ya simu ya mkononi baada ya uvumbuzi imezalisha mabilioni ya fedha (dola) na kuwaokoa mamilioni ya watu, wakiwa nyumbani na kazini, kwa kuwawezesha kuwasiliana popote, wakati wowote na kupata huduma kwa haraka na sahihi.

Mnamo Julai 6, 1971, Mtu mweusi aliyejulikana kama Dr Henry T. Sampson alibuni ” kiini cha umeme wa gamma”, ambayo inawezesha matumizi ya nyuklia (Nuclear Reactor). Kwa mujibu wa Dk Sampson wa Gamma Electric Cell, ugunduzi huo uliwekewa hatimiliki Julai 6, 1971, Patent No 3,591,860 inayozalisha umeme mkubwa na sasa kuchunguza mionzi katika ardhi.

Mgunduzi huyo, alizaliwa eneo la Jackson, Mississippi, akapata Shahada ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Purdue mwaka 1956. Aliendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles ambako alihitimu Shahada ya pili (MSc) katika uhandisi mwaka 1961. Akasoma katika Chuo Kikuu cha Illinois Urbana-Champaign, MS katika Uhandisi nyuklia mwaka 1965, na PhD mwaka 1967.

Image result for dr henry sampson

Mawasiliano ya Simu yalipiga hatua kubwa zaidi mwaka 1983 baada ya Henry T. Sampson kugundua mfumo wa Cellular kurekebisha simu za mkononi, ambayo hutumia mawimbi ya redio kwa kusambaza na kupokea ishara ya kusikiliza.

Kabla ya wakati huo, huduma ya simu nchini Marekani, ilihusisha zaidi simu za kwenye gari, ambazo zilikuwa ndogo sana kwa sababu ya maeneo ya mji mkuu yalikuwa yanatumia antenna moja tu kwa madhumuni haya.

Henry T. Sampson alifanya kazi kama Mhandisi mtafiti wa kemikali katika kituo cha utafiti wa zana za kivita za Majini Marekani (the US Naval Weapons Center ) China Lake, California. mwaka 1956-1961. Baadaye akahamia Aerospace Corp, El Segundo, California.

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Yassir Oyo

Yassir Oyo

Ni Mwandishii wa Taarifa za Teknolojia kwa lugha ya kiswahili katika Mtandao wa Taarifa za Teknolojia - TeknoTaarifa. Naishi Nairobi Kenya, Napenda Teknolojia, Naipenda lugha ya kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!