- Je Google ndio kimbilio unapohitaji kutafuta taarifa kwa haraka? - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

MITANDAO

Je Google ndio kimbilio unapohitaji kutafuta taarifa kwa haraka?

on

Unakumbuka maisha kabala ya Google? ulifanya nini wakati ulihitaji kutafuta taarifa fulani kwa haraka?

Chochote unachokitafuta liwe jina la kitu fulani au jinsi ya kuandika jina fulani au jina la eneo fulani bila shaka ni lazima utafute kwenye Google. Kwa kukadiria Google hushughulikia karibu mambo 40,000 kwa sekunde moja, hiyo ni sawa na mambo bilioni 3.5 kwa siku.

Google sasa imegeuka kuwa sio eneo tu la kutafuta majina lakini pia sehemu muhimu kwa matangazo na mkusanyaji wa taarifa za watu. Kila wakati unapofanya kitu fulani, Google inajua kuhusu tabia zetu.

Google ni nini? kwa kweli neno Google halimaanisha chochote.

Lilitokana na kuandikwa vibaya kwa jina la ‘googol’ Kuna madai kadhaa kuhusu labda vile mhandisi au mwanafunzi aliweza kuibuka na jina hilo. Makosa hayo ya uandishi yalichangia kupatikana nene hilo, na mengine ni historia.

Mwaka 1999 Larry na Sergey walijaribu kuiuza Google kwa dola milioni moja lakini hakuna mtu aliyetaka kuinunua hata licha ya bei kushushwa.Google kwa sasa ina thamani ya dola bilioni 300. Kuna mtu anajutia sana

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!