- Ifahamu Programu Inayowasaidia wazazi kudhibiti simu za watoto wao - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

PROGRAMu

Ifahamu Programu Inayowasaidia wazazi kudhibiti simu za watoto wao

on

Matumizi mabaya ya simu ambayo yamekuwa yakifanywa na watoto wao kwa ajili ya kufanikisha michongo isiyo na tija, kampuni moja ya teknolojia iligundua mfumo unaowawezesha wazazi kufuatilia mwendendo wa simu za watoto wao.

Mfumo huo unaojulikana kwa jina la Belimo, ambao unaweza kufanya kazi kupitia mtandao wa Vodafone, unatoa fursa kwa wazazi kudhibiti muda wa watoto wao kuweza kuwa hewani, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au hata kupiga simu.

Tofauti na mifumo mingine inayojulikana kwa lugha ya kiingereza kama Application, mfumo huu umetengenezwa katika namna ambayo mtoto anayedhibitiwa hawezi kuukataa kwa namna yoyote ile kwani anayekuwa na uwezo wa kuuendesha na kuuamuru ni mzazi anayeamua kuutumia.

Tayari mfumo huu umeshapata umaarufu baada ya kutumika ambapo asasi moja ya nchini Uingereza yenye kujihusisha na masuala ya uzazi na malezi, imeweka bayana mtazamo wake juu ya kuukubali mfumo huu

Chini ya mfumo huu, mzazi anaweza kununua kifurushi ambacho kinajumuisha kadi ya simu ya kawaida tu kama zilivyo zinazotumika kwenye simu hivi sasa, lakini ikiwa imeunganishwa kwenye mfumo huo, na huduma hiyo ni ya kulipia kwa kadiri mtumiaji anavyopenda kuendelea kuitumia.

“Mfumo huu unawezesha wazazi kudhibiti kwa mfano, namba zipi ambazo hawapendi ziwe zinawasiliana na mtoto wao, muda wa kupiga simu, kutuma ujumbe na huduma zingine za simu. Lakini pia, wazazi watakuwa na uwezo wa kusoma ujumbe mfupi wa maneno ulioko kwenye simu za watoto wao, bila kuwa na simu za watoto hao” alisema msemaji mmoja wa kampuni iliyoandaa mfumo huo.

Hatua hii imekuja ikiwa ni katika zama ambazo taasisi kadhaa za kiutafiti zimetanabaisha kuwa, watoto hasa wa kike barani Ulaya, wamekuwa katika shinikizo la kutuma kwa njia mbalimbali, mambo yenye kuhusu maisha yao ya kimapenzi, jambo ambalo limekuwa likiwakwaza wazazi wao huku maadili pia yakizidi kupotea.

Chanzo: newstimes.com

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!