- Fahamu njia rahisi ya Kutoibiwa au kubadilishiwa vifaa vya komyuta yako - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

ELIMU

Fahamu njia rahisi ya Kutoibiwa au kubadilishiwa vifaa vya komyuta yako

on

Leo nitakufahamisha Software maalum kabisa kwa ajili ya kulist/Kuorodhesha kila kilichomo ndani ya Kompyuta yako, kwa majina pamoja na Model zake, hivyo basi unaweza kuvirekodi pembeni hata ktk Diary yako kwa usalama zaidi, ili ikitokea umetofautiana na fundi wako basi unafungua software yako na kisha unaiomba ikuorodheshee vifaa vya Kompyuta yako na hapo utaweza kuhakiki kama ni vilevile ulivyovirekodi mwanzo au sivyo, na mwisho kabisa utafahamu ukweli uko wapi.
Faida zasoftware hii;
  1. Haina saizi kubwa (MB 4.9 tu)
  2. Ni rahisi kutumia
  3. Haina kona nyingi wakati wa kuinstall
Zifuatazo ni hatua za kuinstall (Kupakia);
  1. Download software hapa
  2. Utainstall kama kawaidaRelated image
  3. Wakati wa kuinstall haitaomba password na ni free kabisa
  4. Ukimaliza kuinstall nenda kwenye desktop kisha itafute utaona imeandikwa “Speccy”
  5. Double click/Ibonyeze mara 2 harakaharaka ili kuifungua
  6. Ikifunguka itakuja kama hivi inavyo onekana hapa chini.

Max IT Club speccy

Sasa basi hapo unaweza kuona mwenyewe vitu gani vimeorodheshwa kwa majina, saizi pamoja na modeli zake, Kupitia software hii utoibiwa au kubadilishiwa vifaa vya komyuta yako. kwa mfano; RAM, CPU/PROCESSOR, MOTHERBOARD, STORAGE/HARD DISK.

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!