- Fahamu mambo ya kuzingatia unapotaka kununua kompyuta iliyotumika - Teknotaarifa | Mtandao wa Taarifa za Teknolojia -
-

KOMPYUTA

Fahamu mambo ya kuzingatia unapotaka kununua kompyuta iliyotumika

on

Linapokuja swala la kununua kompyuta iliyotumika ni dhahiri sana lazima panaitajika umakini wa hali ya juu, siku hizi kumekuja mitandao ambayo unaweza kununua vitu hivi bila hata ya kumjua mtu anae kuuzia. Hii inaongeza wasiwasi kwa mnunuzi kutokana na kwamba unakuta humjui mtu anae kuuzia Tofauti na hapo awali watu walikua wanauziana bidhaa wanaojuana tu na usipokua makini unaweza kununua bidhaa ambayo haifai kwa matumizi mengine, 

Leo tunakusaidia katika hilo kwa kukuletea mambo muhimu ya kuzingatia wakati unanua kompyuta iliyotumia. Mambo haya ni muhimu sana kuyangali na unapoweza kufanya hivyo basi utaweza kusogeza karibu uwezekano wa kupata kompyuta inayofaa kwa matumizi yako ya baadae.

Kujua Kompyuta Unayotaka

Kabla ya kununua kompyuta ya aina yoyote ni lazima ujue kwanza ni kompyuta gani unataka na kwa matumizi gani, hii ni muhimu sana kuliko kitu chochote kwani watu hua wanajua wanataka kompyuta tu lakini hawajui wanataka kompyuta ya matumizi gani. Kwa kujua kompyuta unayotaka itakusaidia kujua sifa za kompyuta unayotaka hivyo itakusaidia kurahisisha zoezi zima la kutafuta kompyuta unayotaka.

Angalia Kompyuta hiyo ni ya Mwaka Gani

Jambo lingine ambalo litakurahisishia kupata kompyuta bora ni kuangalia mwaka wa kompyuta hiyo, yaani hapa inamaana mwaka wa kompyuta hiyo kutengenezwa kwani kompyuta nyingi ambazo zinakuwa ni za miaka ya zamani mara nyingi zinakuwa hazina ubora unaotakiwa na ukiangalia kwa makini sana unaweza kukuta kompyuta hiyo inao ubovu flani hivyo ni vyema kuwa makini sana na hilo. Unaweza kununua kompyuta za kuanzia mwaka 2010 na kuendelea kwani hizi angalau huwa zinakuwa na ubora flani, Pia unaweza kutizama mwaka wa kompyuta kwa kuangalia nyuma ya kompyuta au unaweza kutumia (Google) kwa kutafuta jina na model ya kompyuta yako.

Angalia Kompyuta hiyo Imetumika kwa Muda Gani

Ni vizuri na ni jambo la msingi kujua kompyuta unayotaka kununua imetumika kwa muda gani kwani kwa kujua hilo utapata makadirio ya uzima wa kompyuta hiyo, kwa mfano kompyuta iliyotumiaka miaka mitano au kumi uwezekano wa kompyuta hii kuendelea kutumika ni mdogo sana hivyo ni vyema kuangalia hilo. Unaweza kuangalia hili kwa kumuuliza muuzaji kama ni mwaminifu au unaweza kumuuliza kama alinunua kompyuta hiyo ikiwa mpya na kama alinunua ikiwa mpya basi angalia mwaka wa kompyuta hiyo kutengenezwa na hapo utaona kompyuta hiyo imekaa muda gani.

Angalia Vifaa vya Nje (Hardware) vya Kompyuta

Hiyo Kuangalia vifaa vya nje ni kitu cha msingi sana inapokuja katika swala la kununua kompyuta iliyotumika, unaweza kuangalia haya yote kwa hatua, kwa mfano unaweza kuanza kwa kuangalia battery, alafu uka angalia kioo cha kompyuta hiyo kisha ukaangalia sehemu za kuweka flash na sehemu nyingine kama hizo kisha ukamalizia na keyboard na Mouse hili ni la muhimu sana kukumbuka kwani watu wengi huangalia mouse lakini wanasahau kuangalia keyboard hivyo ujikuta wamenunua kompyuta ambayo kuna baadhi ya vibonyezo kwenye keyboard havifanyi kazi kabisa hivyo ni vyema kuwa makini. 

Angalia kwa Makini Kama Kompyuta Hiyo Imefunguliwa

Kama kompyuta hiyo ni laptop ni vyema kuangalia kama imefunguliwa kwani mara nyingi kompyuta nyingi ambazo zimefunguliwa hua na matatizo mengine madogo madogo pia kumbuka kuangalia pembeni kwenye kava la kompyuta hiyo kama kuna michubuko inayosababishwa na ufunguaji holela wa kompyuta hiyo.

Angalia Vifaa vya Ndani vya Kompyuta

Hiyo Kwa kuangalia vifaa vya ndani ikiwa pamoja na sifa za kompyuta hiyo utaweza kukamilisha na kujua kama kompyuta hiyo ni nzima na inafaa wewe kununua. Unaweza kufanya hivyo kwa kuanza kuangalia RAM kisha Hard Drive pamoja na Bios kama haina Password ikiwa pamoja na Motherboard ya Kompyuta yako.

Angalia Kampuni Iliyo Tengeneza Kompyuta Hiyo

Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya makampuni ambayo hayako vizuri sana katika utengenezaji wa kompyuta hivyo ni vyema kuangalia sana unapotaka kununua kompyuta iliyotumika. Ni vizuri kuwa makini sana na kompyuta ambazo zina majina ambayo hayajulikani sana kwani hata upatikanaji wa vifaa vya kompyuta hizo hua ni mgumu sana hivyo ni vyema kuchagua majina ya kompyuta ambazo zinajulikana kwa kiasi flani, hii itakusaidia kupata vifaa vya kompyuta yako hiyo pale inapo haribika.

TOA MAONI YAKO HAPA

comments

About Abdallah Magana

Abdallah Magana

Ni Mhariri mkuu, Mwanzilishi na mmiliki wa Tovuti ya TeknoTaarifa. Naishi Dar es Salaam Tanzania. Lengo langu ni kukupasha Taarifa na Kukuelimisha kuhusu sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!